2. UNAFIKIRI NINI KUHUSU MAHUSANO YALIYOPO KATI YA MAFANIKIO YAKO NA JAMII
INAYOKUZUNGUKA?
1/1/2013
X
Be nson Mw inuka
Industria l Engine e r
MASWALI 15 YANAYOWEZA KUKUFANYA UJIBU SWALI HILO HAPO JUU!
MASWALI:-
1. JE, UNAITAMBUA VIZURI JAMII INAYOKUZUNGUKA?
2. UNAFAHAMU NINI KUHUSU TABIA NA MWENENDO WA JAMII INAYOKUZUNGUKA?
3. UNAFIKIRI UNAWEZA KUJAMIIANA NAYO?
4. UNAAMINI KUWA JAMII INAYOKUZUNGUKA INAWEZA KUWA CHACHU KUBWA KATIKA
KUPATA MAFANIKIO YAKO?
5. JE, JAMII INAYOKUZUNGUKA INAKUTAMBUA?
6. HUENDA JAMII/SEHEMU KUBWA YA JAMII IMEKUTENGA!
7. UNAZIFAHAMU SABABU ZILIZOIFANYA/ZINAZOIFANYA JAMII INAYOKUZUNGUKA
UKUTENGA?
8. WEWE UNAINGILIANA VIPI NA JAMII YAKO?
9. UNAWEZA KUTAMBUA KUWA JAMII YAKO INAHITAJI MTU WA NAMNA IPI? (Kwa mfano,
Watu wakali, wapole, wachangamfu, waongeaji sana, wakimya, walevi, watu wa namna
mbili au zaidi katika hizi?)
10. JE, UMEGUNDUA NINI KUHUSU WEWE NA JAMII YAKO? UNAFIKIRI KUWA WEWE NDIYE
MTU WA NAMNA ILE AMBAYE JAMII YAKO INAMHITAJI?
11. JE WEWE UPO TOFUTI NA MTU YULE AMBAYE JAMII YAKO INAMHITAJI?
12. UNAFIKIRI NINI? WEWE UNAWEZA KUIBADILI JAMII NA KUIFANYA IMHITAJI MTU WA
AINA YAKO AU,JE UNAWEZA KUBADILIKA NA KUWA MTU YULE AMBAYE JAMII YAKO
INAMHITAJI?
13. JE, UNAWEZA KUMUDU KUDUMU KATIKA NAMNA AMBAYO JAMII YAKOINAHITAJI? (Kwa
muda gani?)
3. 14. UNAIHESHIMU VIPI JAMII INAYOKUZUNGUKA?
15. UNAFIKIRI JAMII YAKO INAKUHESHIMU SAWA AU ZAIDI YA VILE WEWE
UNAVYOIHESHIMU? (Kama jamii yako haikuheshimu na au inakuheshimu kwa kiwango
kidogo u kujiuliza kwa nini?)
Zaidi ya 75% ya vitu/mambo unayoyahitaji katika maisha yako hayapo mikononi mwako.
75% ya vitu/mambo hayo yapo mikononi mwa watu wengine(Wanajamii wanaokuzunguka!).
Unaweza kujibu maswa yotekuhusu jamii inayokuzunguka ili uweze kupata mafanikio
unayoyatafuta. Huenda wanajamii wanaokuzunguka hawautambui na hivyo hawajui kama
una mahitaji na vitu/mambo hayo. Juhudi yako pekee juu ya mambo hayo haitakufanya
upate vitu/mambo hayo!
IFAHAMU KWANZA JAMII YAKO!
Huenda wanajamii wengine hawatambui kama wana vitu/mambo unayoyahitaji (Swali la 5, 8
linaweza kukusaidia).
MUHIMU!
Hautakiwi kukosea hapa! Usifanye kosa kwa kuchagua na kuibagua jamii yako. Wapo
wengine wanaichukulia jamii yenye nguvu kuwa akina baba tu, au akina mama tu, au vijana
tu, au wazee tu, au watu wakubwa tu na si watoto, au watu flaniflani tu wenye uwezo wa
kiuchumi au kielimu.
Ukifanya hivyo itakuwa vigumu kupata kile unataka kutoka kwa jamii yako.
Jamiii yako yenye nguvu ni muunganiko wa watoto, vijana na wazee,akina mama na akina
baba, walemavu na watu wazima wasio na ulemavu wa aina yoyote, masikini na matajiri,
waliosoma na wasiosoma, wenye nyadhifa na vyeo na wale wasio navyo!
Swali namba 6, 7 na 14.
Huenda watoto au vijana au wazee na au wengine katika makundi hapo juu wamekutenga
na ndio maana umekosa kabisa au umepata sehemu ndogo tu ya hazina waliyonayo ambayo
ndiyo hitaji lako.
Huenda wewe mwenyewe ndio chanzo kilichoifanya jamii ikutenge. Labda wewe mwenyewe
umeanzanakuwatenga watoto, wazee, walemavu, akina mama au akina baba. Labda tabia na
mwenendo wako haujakubalika katika jamii inayokuzunguka!
Huenda kauli na semi zako hazina radha nzuri na kuwavutia wanajamii wanaokuzunguka!
Au labda jamii inayokuzunguka haijakutambua! Unafikiri unahitaji kipaza sauti na
kujitambulisha kwa wanajamii? Benson Mwinuka(Author)
4. KUHUSU MWANDISHI
Benson Mwinuka ni kijana (1989) mwanafunzi anayesomea digrii yake ya kwanza ya Uinjinia
wa viwanda kwa miaka 2011-2015 katika chuo kikuu cha Dar es salaam Nchini Tanzania.
Mara nyingi anatumia muda wake wa ziada kuandaa na kuchapisha nakala mbalimbali zenye
ujumbe na kuelimisha jamii.
Ameshafanya nakala ya Wakati wa kufanya mabadiliko, nakala ya “What’s all about a
chance?” na nyingine nyingi zinazoambatana na hii.
“Je unitambua vizuri jamii inayokuzunguka?”
MAWASILIANO:-
E-mail: beniefaith@gmail.com
Phone:-
Line 1: +255768 661 416
Line 2: +255719 288 419
Blog: http//www.tanzania-nyumbani.blogspot.com