SlideShare uma empresa Scribd logo
1 de 3
FASIHI YA KISWAHILI
KARATASI YA PILI
320/2
TAMTHILIA
Tamthilia ni nini?
• Tamthilia ni utanzu wa fasihi ambao huwasilishwa kupitia mazungumzo
na uigizaji ili kuwasilisha ujumbe wake. Kulingana na Wamitila (2007)
huu ni utanzu ambao huandikwa kwa mtindo wa mazungumzo ya
wahusika.
• Nkwera (h.t) anaelezea kuwa tamthilia ni: “Tamthilia ni mchezo wa
kuigiza au utungo wa kisanaa ambao huweka wazo fulani katika
matendo na mazungumzo” (Nkwera, h.t)
• Tamthilia (pia: Tamthiliya au Tamthilia-Mchezo) ni moja kati ya
sehemu ya utunzi wa hadithi au fasihi simulizi (ngano au hadithi)
ambayo mara nyingi tunaona kupitia katika makumbi au televisheni,
kusikia kupitia katika redio.
• Tamthilia au mchezo mara nyingi huwa mazunguzo baina ya watu, na
kwa kawaida huwa mchezo hatuutizami katika TV tu, bali hata kuna
watu wengine hufuatilia kwa kupitia maandiko yenye tamthiliya hizo
na kuzielewa vyema.
• Watu tunaowaona wanafanya tamthilia ni waigizaji; katika ukumbi
wa maonyesho husimama juu ya jukwaa na kuanza kutoa burudani
huku watu wakiwaangalia (watazamaji) wanaweza wakawaona vyema
kabisa.
• Mwongozaji ana wasaidia waigizaji waigizaji kufanya kazi zao vyema,
au anawaeleza namna ya mchezo jinsi vile unavyotakiwa kuchezwa.
AINA ZA TAMTHILIA
Kuna aina nyingi ya michezo au tamthiliya, kama vile;
1. Tamthilia Cheshi/Komedia - ni mchezo wa kuchekesha. Maudhui
yake huundwa kwa lengo la kutumbuiza hadhira.
2. Tamthilia Simanzi/Trejedia - ni mchezo uliojaa huzuni, mikasa,
mikosi, visa vya kutisha na aghalabu baadhi ya wahusika wakuu hufa.
1
3. Tamthilia Simanzi-Cheshi/Trejikomedia - ni mchezo wenye visa
vya kuhuzunisha lakini pia unawasilisha kwa njia ya kuchekesha.
Aghalabu wahusika hutumia kejeli kuchekesha hadhira ijapokuwa kuna
shida fulani inayowakabili. Baadhi ya wahusika wakuu hukumbwa na
mikasa.
Mfano: Kifo Kisimani (na Kithaka Wa Mberia)
4. Tamthilia Tatizo - ni mchezo wa kuigiza ambapo wahusika huwa na
tatizo/shida kuu wanalotaka kulitatua. Tamthilia hii aghalabu hutumia
mbinu ya taharuki ili kuwafanya hadhira wawe makini ili kuona jinsi
tatizo hilo litakavyoishia.
5. Tamthilia ya Domestiki Drama - ni mchezo unaoangazia maisha
ya kawaida ya watu kama vile familia, urafiki, ndoa n.k
6. Tamthilia ya Melodrama - ni mchezo ambao husisitiza sifa za
wahusika kwa kuunda wahusika kuunda wahusika wenye sifa
zilizopigiwa chuku na zisizobadilika. Tamthilia hizi huundwa kwa
namna inayowafanya hadhira wawapende wahusika fulani na
wawachukie wahusika wengine. Kwa mfano:
• Shujaa ambaye hushinda kila mara.
• Wahusika wabaya ambao hubakia wabaya kutoka mwanzo
hadi mwishi.
• Wahusika wazuri ambao hufanya vitendo vizuri kutoka
mwanzo hadi mwisho.
• Wapenzi ambao hata wakitenganishwa bado watapendana
• Aghalabu huishia kwa raha mustarehe.
7. Tamthilia Tanzia /Trejidia - huu ni mchezo wa huzuni tu, kwa
sababu ya mikosi na nuksi iliyomo. Mara nyingi aina ya tamthilia hii
huwa na mwisho mbaya au wa huzuni na wenye kutisha sana.
MAUDHUI YA TAMTHILIA
Maudhui ya tamthilia yanagusia vipengele vya: migogoro, ujumbe,
falsafa, mtazamo, msimamo, na dhamira.
DHAMIRA YA TAMTHILIA
Matumizi ya tamthilia ni pamoja na: kuelimisha jamii; (katika masuala
mbalimbali kama vile: uchumi, siasa, maadili, nk.) kuburudisha jamii,
kuonya na kukosoa jamii, kukuza lugha, kurithisha amali za jamii (mila
na desturi za jamii husika), nk.
2
3

Mais conteúdo relacionado

Mais procurados

Matumizi ya Lugha Kimuktadha
Matumizi ya Lugha KimuktadhaMatumizi ya Lugha Kimuktadha
Matumizi ya Lugha Kimuktadhamussa Shekinyashi
 
Umuhimu wa kujifunza nadharia za fonolojia
Umuhimu wa kujifunza nadharia za fonolojiaUmuhimu wa kujifunza nadharia za fonolojia
Umuhimu wa kujifunza nadharia za fonolojiaHamad Khamis Juma
 
Using drama in the classroom
Using drama in the classroomUsing drama in the classroom
Using drama in the classroomInma Garín
 
hymes and bachman's theories/model of communicative competence
hymes and bachman's theories/model of communicative competencehymes and bachman's theories/model of communicative competence
hymes and bachman's theories/model of communicative competenceMia de Guzman
 
Relationship between language, culture, and identity
Relationship between language, culture, and identityRelationship between language, culture, and identity
Relationship between language, culture, and identityCool Chaandni
 
Language, dialect, and varieties
Language, dialect, and varietiesLanguage, dialect, and varieties
Language, dialect, and varietiesSari Kusumaningrum
 
Language As Symbols
Language As  SymbolsLanguage As  Symbols
Language As Symbolsplisasm
 
The concept of sociolinguistics
The concept of sociolinguisticsThe concept of sociolinguistics
The concept of sociolinguisticsaab1984
 
Gender Issues In Classroom and Society.pptx
Gender Issues In Classroom and Society.pptxGender Issues In Classroom and Society.pptx
Gender Issues In Classroom and Society.pptxJawad Ahmed
 
Grammaticality & Acceptability
Grammaticality & AcceptabilityGrammaticality & Acceptability
Grammaticality & AcceptabilityAnusha Das
 
Characteristics of human language
Characteristics of human languageCharacteristics of human language
Characteristics of human languageAlan Bessette
 

Mais procurados (20)

TAFSIRI NA UKALIMANI
TAFSIRI NA UKALIMANITAFSIRI NA UKALIMANI
TAFSIRI NA UKALIMANI
 
UTUMIZI WA LUGHA
UTUMIZI WA LUGHAUTUMIZI WA LUGHA
UTUMIZI WA LUGHA
 
Uhifadhi wa fasihi simulizi
Uhifadhi wa fasihi simuliziUhifadhi wa fasihi simulizi
Uhifadhi wa fasihi simulizi
 
UTUNGAJI
UTUNGAJIUTUNGAJI
UTUNGAJI
 
MATUMIZI YA SARUFI
MATUMIZI YA SARUFIMATUMIZI YA SARUFI
MATUMIZI YA SARUFI
 
Mjengo wa tungo 3
Mjengo wa tungo 3Mjengo wa tungo 3
Mjengo wa tungo 3
 
Sarufi Matamshi (Fonolojia)
Sarufi Matamshi (Fonolojia)Sarufi Matamshi (Fonolojia)
Sarufi Matamshi (Fonolojia)
 
Matumizi ya Lugha Kimuktadha
Matumizi ya Lugha KimuktadhaMatumizi ya Lugha Kimuktadha
Matumizi ya Lugha Kimuktadha
 
Umuhimu wa kujifunza nadharia za fonolojia
Umuhimu wa kujifunza nadharia za fonolojiaUmuhimu wa kujifunza nadharia za fonolojia
Umuhimu wa kujifunza nadharia za fonolojia
 
Using drama in the classroom
Using drama in the classroomUsing drama in the classroom
Using drama in the classroom
 
hymes and bachman's theories/model of communicative competence
hymes and bachman's theories/model of communicative competencehymes and bachman's theories/model of communicative competence
hymes and bachman's theories/model of communicative competence
 
Relationship between language, culture, and identity
Relationship between language, culture, and identityRelationship between language, culture, and identity
Relationship between language, culture, and identity
 
Language, dialect, and varieties
Language, dialect, and varietiesLanguage, dialect, and varieties
Language, dialect, and varieties
 
Language As Symbols
Language As  SymbolsLanguage As  Symbols
Language As Symbols
 
The history of drama
The history of dramaThe history of drama
The history of drama
 
The concept of sociolinguistics
The concept of sociolinguisticsThe concept of sociolinguistics
The concept of sociolinguistics
 
Gender Issues In Classroom and Society.pptx
Gender Issues In Classroom and Society.pptxGender Issues In Classroom and Society.pptx
Gender Issues In Classroom and Society.pptx
 
Grammaticality & Acceptability
Grammaticality & AcceptabilityGrammaticality & Acceptability
Grammaticality & Acceptability
 
Genre Analysis
Genre AnalysisGenre Analysis
Genre Analysis
 
Characteristics of human language
Characteristics of human languageCharacteristics of human language
Characteristics of human language
 

Destaque

KISWAHILI Paper 336/1 O'Level Exams.
KISWAHILI Paper 336/1 O'Level Exams.KISWAHILI Paper 336/1 O'Level Exams.
KISWAHILI Paper 336/1 O'Level Exams.Ignatius Ntungwa
 
Paper 336 s.2 mid term 2015
Paper 336 s.2 mid term 2015Paper 336 s.2 mid term 2015
Paper 336 s.2 mid term 2015Ignatius Ntungwa
 
The Standard: Enock Maregesi
The Standard: Enock MaregesiThe Standard: Enock Maregesi
The Standard: Enock MaregesiEnock Maregesi
 
2015 Upload Campaigns Calendar - SlideShare
2015 Upload Campaigns Calendar - SlideShare2015 Upload Campaigns Calendar - SlideShare
2015 Upload Campaigns Calendar - SlideShareSlideShare
 
What to Upload to SlideShare
What to Upload to SlideShareWhat to Upload to SlideShare
What to Upload to SlideShareSlideShare
 
Getting Started With SlideShare
Getting Started With SlideShareGetting Started With SlideShare
Getting Started With SlideShareSlideShare
 

Destaque (9)

KISWAHILI Paper 336/1 O'Level Exams.
KISWAHILI Paper 336/1 O'Level Exams.KISWAHILI Paper 336/1 O'Level Exams.
KISWAHILI Paper 336/1 O'Level Exams.
 
UTAFITI WA KIELIMU
UTAFITI  WA KIELIMUUTAFITI  WA KIELIMU
UTAFITI WA KIELIMU
 
Paper 336 s.2 mid term 2015
Paper 336 s.2 mid term 2015Paper 336 s.2 mid term 2015
Paper 336 s.2 mid term 2015
 
Tamthilia MAMA Ee
Tamthilia MAMA EeTamthilia MAMA Ee
Tamthilia MAMA Ee
 
Maana ya maana!
Maana ya maana!Maana ya maana!
Maana ya maana!
 
The Standard: Enock Maregesi
The Standard: Enock MaregesiThe Standard: Enock Maregesi
The Standard: Enock Maregesi
 
2015 Upload Campaigns Calendar - SlideShare
2015 Upload Campaigns Calendar - SlideShare2015 Upload Campaigns Calendar - SlideShare
2015 Upload Campaigns Calendar - SlideShare
 
What to Upload to SlideShare
What to Upload to SlideShareWhat to Upload to SlideShare
What to Upload to SlideShare
 
Getting Started With SlideShare
Getting Started With SlideShareGetting Started With SlideShare
Getting Started With SlideShare
 

Tamthilia ni nini?

  • 1. FASIHI YA KISWAHILI KARATASI YA PILI 320/2 TAMTHILIA Tamthilia ni nini? • Tamthilia ni utanzu wa fasihi ambao huwasilishwa kupitia mazungumzo na uigizaji ili kuwasilisha ujumbe wake. Kulingana na Wamitila (2007) huu ni utanzu ambao huandikwa kwa mtindo wa mazungumzo ya wahusika. • Nkwera (h.t) anaelezea kuwa tamthilia ni: “Tamthilia ni mchezo wa kuigiza au utungo wa kisanaa ambao huweka wazo fulani katika matendo na mazungumzo” (Nkwera, h.t) • Tamthilia (pia: Tamthiliya au Tamthilia-Mchezo) ni moja kati ya sehemu ya utunzi wa hadithi au fasihi simulizi (ngano au hadithi) ambayo mara nyingi tunaona kupitia katika makumbi au televisheni, kusikia kupitia katika redio. • Tamthilia au mchezo mara nyingi huwa mazunguzo baina ya watu, na kwa kawaida huwa mchezo hatuutizami katika TV tu, bali hata kuna watu wengine hufuatilia kwa kupitia maandiko yenye tamthiliya hizo na kuzielewa vyema. • Watu tunaowaona wanafanya tamthilia ni waigizaji; katika ukumbi wa maonyesho husimama juu ya jukwaa na kuanza kutoa burudani huku watu wakiwaangalia (watazamaji) wanaweza wakawaona vyema kabisa. • Mwongozaji ana wasaidia waigizaji waigizaji kufanya kazi zao vyema, au anawaeleza namna ya mchezo jinsi vile unavyotakiwa kuchezwa. AINA ZA TAMTHILIA Kuna aina nyingi ya michezo au tamthiliya, kama vile; 1. Tamthilia Cheshi/Komedia - ni mchezo wa kuchekesha. Maudhui yake huundwa kwa lengo la kutumbuiza hadhira. 2. Tamthilia Simanzi/Trejedia - ni mchezo uliojaa huzuni, mikasa, mikosi, visa vya kutisha na aghalabu baadhi ya wahusika wakuu hufa. 1
  • 2. 3. Tamthilia Simanzi-Cheshi/Trejikomedia - ni mchezo wenye visa vya kuhuzunisha lakini pia unawasilisha kwa njia ya kuchekesha. Aghalabu wahusika hutumia kejeli kuchekesha hadhira ijapokuwa kuna shida fulani inayowakabili. Baadhi ya wahusika wakuu hukumbwa na mikasa. Mfano: Kifo Kisimani (na Kithaka Wa Mberia) 4. Tamthilia Tatizo - ni mchezo wa kuigiza ambapo wahusika huwa na tatizo/shida kuu wanalotaka kulitatua. Tamthilia hii aghalabu hutumia mbinu ya taharuki ili kuwafanya hadhira wawe makini ili kuona jinsi tatizo hilo litakavyoishia. 5. Tamthilia ya Domestiki Drama - ni mchezo unaoangazia maisha ya kawaida ya watu kama vile familia, urafiki, ndoa n.k 6. Tamthilia ya Melodrama - ni mchezo ambao husisitiza sifa za wahusika kwa kuunda wahusika kuunda wahusika wenye sifa zilizopigiwa chuku na zisizobadilika. Tamthilia hizi huundwa kwa namna inayowafanya hadhira wawapende wahusika fulani na wawachukie wahusika wengine. Kwa mfano: • Shujaa ambaye hushinda kila mara. • Wahusika wabaya ambao hubakia wabaya kutoka mwanzo hadi mwishi. • Wahusika wazuri ambao hufanya vitendo vizuri kutoka mwanzo hadi mwisho. • Wapenzi ambao hata wakitenganishwa bado watapendana • Aghalabu huishia kwa raha mustarehe. 7. Tamthilia Tanzia /Trejidia - huu ni mchezo wa huzuni tu, kwa sababu ya mikosi na nuksi iliyomo. Mara nyingi aina ya tamthilia hii huwa na mwisho mbaya au wa huzuni na wenye kutisha sana. MAUDHUI YA TAMTHILIA Maudhui ya tamthilia yanagusia vipengele vya: migogoro, ujumbe, falsafa, mtazamo, msimamo, na dhamira. DHAMIRA YA TAMTHILIA Matumizi ya tamthilia ni pamoja na: kuelimisha jamii; (katika masuala mbalimbali kama vile: uchumi, siasa, maadili, nk.) kuburudisha jamii, kuonya na kukosoa jamii, kukuza lugha, kurithisha amali za jamii (mila na desturi za jamii husika), nk. 2
  • 3. 3