SlideShare uma empresa Scribd logo
1 de 28
ENOCK MAREGESI
MSHINDI WA PILI WA TUZO YA
KISWAHILI YA MABATI-CORNELL YA
FASIHI YA KIAFRIKA 2015
MWANDISHI WA KOLONIA SANTITA
MAHOJIANO
Ulianzaje kuandika?
Nilianza kuandika kwa kujijengea
utamaduni. Utamaduni wa kuandika.
Popote pale nilipoona kitu ambacho
nilidhani kilifaa kuandikwa mahali,
nilikiandika bila kusita au kuchelewa kwa
namna yoyote ile. Nilianza kwa kuandika
insha na kitu chochote kile kama vile
barua kwa rafiki yangu wa kike wa
kipindi kile, marafiki na kwa familia
yangu pia. Hicho ndicho kilichoniingiza
katika biashara hii ya uandishi wa vitabu.
Hadithi yangu ya kwanza kabisa
kuandika iliitwa Magaidi wa
Namba One – Namba One likiwa
jina la sehemu – hadithi fupi ya
kijasusi iliyohusu genge la
kijambazi, lililokuwa na maskani
yake mjini Dodoma. Magaidi wa
Namba One ilikuwa na urefu wa
kurasa 15. Niliiandika nikiwa na
umri wa miaka 15 au 16 hivi, katika
Shule ya Sekondari ya Bihawana ya
mkoani Dodoma.
Hadithi hii ilihusu kikundi cha
kigaidi kilichoitwa Namba One.
Kikundi hiki kilikuwa na makao yake
makuu nje ya Dodoma, katika pori
la Namba One, kama unaelekea
Iringa. Lilifanya shughuli zake ndani
na nje ya Dodoma hadi siku moja
mkubwa wake alipokamatwa; na
baadaye kupata adhabu ya kifungo
cha maisha jela kilichoambatana na
kazi ngumu, katika gereza lenye
ulinzi mkali la mkoani Shinyanga.
Baada ya hapo, viongozi wote wakubwa
wa kikundi hicho walikamatwa na
kukabidhiwa vifungo kulingana na
makosa waliyoyafanya.
Nini kilikusukuma kuwa mwandishi wa vitabu?
Nilihamasishwa na watu wengi na
matukio mengi kuwa mwandishi wa
vitabu: Ngugi wa Thiong’o, Ben Mtobwa,
Euphrase Kezilahabi, Penina Mlama,
Shafi Adam Shafi, sinema za mapigano
kama vile The Big Boss ya Bruce Lee na
Missing in Action ya Chuck Norris,
hadithi kutoka kwa wazee na watu
wengine wakubwa, na kadhalika.
Hata hivyo, hamasa kubwa zaidi
kushinda zote ilitoka kwa Shaaban
Robert – mzalendo wa kweli wa
Tanzania na kinara wa lugha ya
Kiswahili – ambaye vitabu vyake vilinipa
nguvu (na tumaini) kuandika riwaya
yangu ya kwanza ya Kolonia Santita,
ambayo awali iliitwa Salina Cruz.
Salina Cruz ni mji wa mwambao wa
kusini-magharibi mwa Meksiko,
katika jimbo la Oaxaca, kateli ya
Kolonia Santita ilipoanzishwa.
Nilipomaliza masomo yangu ya
sekondari mwaka 1992 nilianza kuandika
Kolonia Santita. Kipindi hicho nilikuwa
nikisubiri majibu ya mtihani wa taifa wa
kidato cha nne. Siku moja (nilipoanza
rasmi kuandika, miaka 23 iliyopita)
niliijiwa ghafla na ndoto ya mchana
nikiwa katika bustani ya nyumbani kwetu
Kijitonyama, Dar es Salaam. Vita kubwa
ya mawazo iliendelea kichwani mwangu
kwa muda mrefu bila kukoma, kuhusiana
na dhana fulani ambayo nilikuwa bado
sijaielewa sawasawa.
Ndoto hiyo ikawa msingi wa taaluma
yangu ya uandishi wa vitabu na msingi
wa utetezi wangu wa lugha ya Kiswahili.
Ikanikumbusha uzuri wa kipaji na uwezo
wa talanta nilivyopewa na Mungu na
jinsi gani nivitumie, na ikanikumbusha
jinsi gani nilivyoweza kuwa na uwezo
mkubwa kuburudisha na kuelimisha
watu kwa nguvu ya neno.
Ujasiri wa kujaribu au jeuri ya kufanya
kitu na kujiamini na tumaini, ulinipa
msingi wa kufikiri vyema na kuandika
kwenye karatasi dhana mbalimbali na
mawazo kadha wa kadha kutoka katika
dunia niliyoigundua. Nilikuwa na
uwezo, nilidhani, wa kuwa mojawapo
kati ya watoa burudani bora na
waandishi bora wa vitabu Tanzania.
Bustanini nilitamani sana kuchapisha
kitabu changu nje ya Tanzania na Afrika,
mathalani Uingereza au Marekani,
ambapo uchapishaji wa vitabu ni wa
kimataifa na wa daraja la kwanza.
Kichwa changu kilifikiria riwaya ambayo
ingesimulia mandhari ya miji zaidi ya
minne ulimwenguni kote, ambayo
baadaye ingekuwa ya kwanza kwa
mauzo hapa Afrika ya Mashariki na Kati.
Nilitamani hadithi yangu
ichapishwe nje kupata ubora wa
kitabu, na ubora wa huduma za
uchapishaji wa vitabu.
Hadithi ya Kolonia Santita niliiandika kwa
miezi mitatu mfululizo hadi
nilipokamilisha rasimu ya kwanza kabisa
ya muswada wenyewe. (Nilikuwa na
umri wa miaka 20 nilipofanya hivyo). Kila
nilipodhani muswada umekamilika ili
niupeleke kwa wachapishaji, niligundua
bado ulihitaji marekebisho.
Mwaka 1999 hata hivyo nilidhani
umekamilika, na niliupeleka Popular
Publications Ltd (PPL) kwa ajili ya
mkataba wa uchapishaji wa vitabu.
Lakini PPL waliukataa muswada huo.
Waliukataa kutokana na ripoti iliyokuwa
na mchango mkubwa kwangu ya Hayati
Saifu D. Kiango, ambaye kipindi hicho
alikuwa mhariri mwandamizi wa Baraza
la Kiswahili la Tanzania (BAKITA).
Kiango alishauri katika ripoti yake
masahihisho mengi katika muswada
wangu, ambayo yote nilikubaliana nayo,
kabla sijaurudisha kwa wachapishaji
lakini nikashindwa kufanya hivyo.
Nilishindwa kuurudisha kwa
wachapishaji.
PPL walipoteza baadhi ya sura za
muswada wa Kolonia Santita (sura ya 7,
8 na 9) na sikufurahishwa na majibu
niliyopewa na Ndg. Mhando (nimesahau
majina yake mengine) kwamba
yeye/ofisi hawakujua hizo sura
zilipokwenda na kwamba yeye/ofisi
walipeleka muswada BAKITA ukiwa
umekamilika kabisa. Mhando alikuwa
mhariri mwandamizi wa PPL.
Kwa sababu hiyo niliuondoa
muswada wangu PPL na kuweka
nadhiri ya kusahihisha kila kosa
aliloliona Kiango na kushauri
nilisahihishe, na nadhiri ya
kuchapisha kitabu hicho mimi
mwenyewe nje ya Afrika kama
ningepata nafasi.
Mnamo mwaka 1992 hadi 1999 nilipata
nafasi ya kuandika miswada mingine
mitano. Miwili kati ya miswada hiyo
ilikuwa imekamilika. Mitatu ilikuwa
bado. Mitatu ni ya kipelelezi. Miwili ni ya
kimapenzi. Septemba 2004 nilihamia
London nchini Uingereza. Huko nilipata
nafasi nzuri zaidi ya kufanya utafiti
yakinifu, wa miswada yangu yote sita,
kwa kiwango nilichokitaka.
Katika maisha yangu yote
nilitamani sana kuwa mtetezi wa
lugha na utamaduni wa Kiswahili.
Nadhani tunahitaji wote kuwa
watetezi wa lugha hii na lugha
zingine za Kiafrika kwani hizi ndiyo
utambulisho wa bara letu.
Kutokana na hamu hiyo, mwaka
1995 niliweka nadhiri ya kupigania
lugha ya Kiswahili maisha yangu
yote yaliyobakia. Lakini nilijua hilo
lisingewezekana bila kwanza
kufanikisha elimu.
Mwaka 2010 nilijiunga na chuo cha
ubunifu wa kifasihi cha Manchester (The
Writers Bureau) nchini Uingereza, kwa
lengo la kutimiza ndoto zangu na kupata
taaluma ya uandishi wa vitabu. The
Writers Bureau walinipa moyo wa
kujiamini. Nilikuwa nikiishi shimoni,
gizani. Hata hivyo, baada ya kupitia
vitabu vichache vya kozi niliona nuru
upande wa pili wa tobwe.
Nilijua, kutokea kipindi hicho kwamba,
endapo ningesoma kwa bidii ningepata
uzoefu na utaalamu na mwongozo hasa
niliyoutaka. Nilitamani kuwa
mwandishi bora wa vitabu na
nilitamani kuwaelimisha watu na
kuwaburudisha pia. Nilitamani kuwa
mojawapo ya waandishi bora wa vitabu
na wauzaji bora wa vitabu nchini
Tanzania, na nje ya hapo.
Ulishindaje?
Habari ya Tuzo ya Kiswahili ya Mabati-Cornell
ya Fasihi ya Kiafrika niliipata kwa mshangao
mkubwa. Kwanza, niliipata kutoka kwa
Mkurugenzi wa CDEA (Culture for Development
East Africa) Ayeta Anne Wangusa mwezi wa
tatu 2015 ofisini kwake Dar es Salaam. Kisha
nikaandaa muswada wangu vizuri na kuutuma
kupitia tovuti ya tuzo kwa waamuzi wa tuzo,
kwa ajili ya mashindano.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya
Tuzo ya Kiswahili ya Mabati-Cornell ya
Fasihi ya Kiafrika Profesa Abdillatif
Abdalla aliponipigia simu kunijulisha
kwamba muswada wangu ulishinda
nafasi ya pili nilifurahi sana. Nilifurahi
sana kiasi kwamba nilijifungia chumbani
kwangu hotelini na kucheza muziki kwa
masaa matatu mfululizo, na nimekuwa
na furaha kuanzia kipindi hicho na
kuendelea.
Sababu kubwa ya muswada wangu
kushinda ni kujitahidi kwa kadiri ya
uwezo wangu WOTE. Ni uvumilivu,
uchapakazi na nidhamu.
Nini ushauri wako kwa waandishi chipukizi?
Ushauri wangu pekee ninaoweza
kutoa kwa waandishi chipukizi ni
elimu! Hutaweza kufikia malengo
yako kikamilifu bila msaada wa
wataalamu – Hata kama una kipaji
au ujuzi kiasi gani.
Ukiwa na kipaji nenda shule kurekebisha
kipaji chako, ukiwa na ujuzi nenda shule
kurekebisha ujuzi wako.

Mais conteúdo relacionado

Destaque

2024 State of Marketing Report – by Hubspot
2024 State of Marketing Report – by Hubspot2024 State of Marketing Report – by Hubspot
2024 State of Marketing Report – by HubspotMarius Sescu
 
Everything You Need To Know About ChatGPT
Everything You Need To Know About ChatGPTEverything You Need To Know About ChatGPT
Everything You Need To Know About ChatGPTExpeed Software
 
Product Design Trends in 2024 | Teenage Engineerings
Product Design Trends in 2024 | Teenage EngineeringsProduct Design Trends in 2024 | Teenage Engineerings
Product Design Trends in 2024 | Teenage EngineeringsPixeldarts
 
How Race, Age and Gender Shape Attitudes Towards Mental Health
How Race, Age and Gender Shape Attitudes Towards Mental HealthHow Race, Age and Gender Shape Attitudes Towards Mental Health
How Race, Age and Gender Shape Attitudes Towards Mental HealthThinkNow
 
AI Trends in Creative Operations 2024 by Artwork Flow.pdf
AI Trends in Creative Operations 2024 by Artwork Flow.pdfAI Trends in Creative Operations 2024 by Artwork Flow.pdf
AI Trends in Creative Operations 2024 by Artwork Flow.pdfmarketingartwork
 
PEPSICO Presentation to CAGNY Conference Feb 2024
PEPSICO Presentation to CAGNY Conference Feb 2024PEPSICO Presentation to CAGNY Conference Feb 2024
PEPSICO Presentation to CAGNY Conference Feb 2024Neil Kimberley
 
Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)
Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)
Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)contently
 
How to Prepare For a Successful Job Search for 2024
How to Prepare For a Successful Job Search for 2024How to Prepare For a Successful Job Search for 2024
How to Prepare For a Successful Job Search for 2024Albert Qian
 
Social Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie Insights
Social Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie InsightsSocial Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie Insights
Social Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie InsightsKurio // The Social Media Age(ncy)
 
Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024
Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024
Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024Search Engine Journal
 
5 Public speaking tips from TED - Visualized summary
5 Public speaking tips from TED - Visualized summary5 Public speaking tips from TED - Visualized summary
5 Public speaking tips from TED - Visualized summarySpeakerHub
 
ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd
ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd
ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd Clark Boyd
 
Getting into the tech field. what next
Getting into the tech field. what next Getting into the tech field. what next
Getting into the tech field. what next Tessa Mero
 
Google's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search Intent
Google's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search IntentGoogle's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search Intent
Google's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search IntentLily Ray
 
Time Management & Productivity - Best Practices
Time Management & Productivity -  Best PracticesTime Management & Productivity -  Best Practices
Time Management & Productivity - Best PracticesVit Horky
 
The six step guide to practical project management
The six step guide to practical project managementThe six step guide to practical project management
The six step guide to practical project managementMindGenius
 
Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...
Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...
Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...RachelPearson36
 

Destaque (20)

2024 State of Marketing Report – by Hubspot
2024 State of Marketing Report – by Hubspot2024 State of Marketing Report – by Hubspot
2024 State of Marketing Report – by Hubspot
 
Everything You Need To Know About ChatGPT
Everything You Need To Know About ChatGPTEverything You Need To Know About ChatGPT
Everything You Need To Know About ChatGPT
 
Product Design Trends in 2024 | Teenage Engineerings
Product Design Trends in 2024 | Teenage EngineeringsProduct Design Trends in 2024 | Teenage Engineerings
Product Design Trends in 2024 | Teenage Engineerings
 
How Race, Age and Gender Shape Attitudes Towards Mental Health
How Race, Age and Gender Shape Attitudes Towards Mental HealthHow Race, Age and Gender Shape Attitudes Towards Mental Health
How Race, Age and Gender Shape Attitudes Towards Mental Health
 
AI Trends in Creative Operations 2024 by Artwork Flow.pdf
AI Trends in Creative Operations 2024 by Artwork Flow.pdfAI Trends in Creative Operations 2024 by Artwork Flow.pdf
AI Trends in Creative Operations 2024 by Artwork Flow.pdf
 
Skeleton Culture Code
Skeleton Culture CodeSkeleton Culture Code
Skeleton Culture Code
 
PEPSICO Presentation to CAGNY Conference Feb 2024
PEPSICO Presentation to CAGNY Conference Feb 2024PEPSICO Presentation to CAGNY Conference Feb 2024
PEPSICO Presentation to CAGNY Conference Feb 2024
 
Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)
Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)
Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)
 
How to Prepare For a Successful Job Search for 2024
How to Prepare For a Successful Job Search for 2024How to Prepare For a Successful Job Search for 2024
How to Prepare For a Successful Job Search for 2024
 
Social Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie Insights
Social Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie InsightsSocial Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie Insights
Social Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie Insights
 
Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024
Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024
Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024
 
5 Public speaking tips from TED - Visualized summary
5 Public speaking tips from TED - Visualized summary5 Public speaking tips from TED - Visualized summary
5 Public speaking tips from TED - Visualized summary
 
ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd
ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd
ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd
 
Getting into the tech field. what next
Getting into the tech field. what next Getting into the tech field. what next
Getting into the tech field. what next
 
Google's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search Intent
Google's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search IntentGoogle's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search Intent
Google's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search Intent
 
How to have difficult conversations
How to have difficult conversations How to have difficult conversations
How to have difficult conversations
 
Introduction to Data Science
Introduction to Data ScienceIntroduction to Data Science
Introduction to Data Science
 
Time Management & Productivity - Best Practices
Time Management & Productivity -  Best PracticesTime Management & Productivity -  Best Practices
Time Management & Productivity - Best Practices
 
The six step guide to practical project management
The six step guide to practical project managementThe six step guide to practical project management
The six step guide to practical project management
 
Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...
Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...
Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...
 

The Standard: Enock Maregesi

  • 1. ENOCK MAREGESI MSHINDI WA PILI WA TUZO YA KISWAHILI YA MABATI-CORNELL YA FASIHI YA KIAFRIKA 2015 MWANDISHI WA KOLONIA SANTITA MAHOJIANO
  • 2. Ulianzaje kuandika? Nilianza kuandika kwa kujijengea utamaduni. Utamaduni wa kuandika. Popote pale nilipoona kitu ambacho nilidhani kilifaa kuandikwa mahali, nilikiandika bila kusita au kuchelewa kwa namna yoyote ile. Nilianza kwa kuandika insha na kitu chochote kile kama vile barua kwa rafiki yangu wa kike wa kipindi kile, marafiki na kwa familia yangu pia. Hicho ndicho kilichoniingiza katika biashara hii ya uandishi wa vitabu.
  • 3. Hadithi yangu ya kwanza kabisa kuandika iliitwa Magaidi wa Namba One – Namba One likiwa jina la sehemu – hadithi fupi ya kijasusi iliyohusu genge la kijambazi, lililokuwa na maskani yake mjini Dodoma. Magaidi wa Namba One ilikuwa na urefu wa kurasa 15. Niliiandika nikiwa na umri wa miaka 15 au 16 hivi, katika Shule ya Sekondari ya Bihawana ya mkoani Dodoma.
  • 4. Hadithi hii ilihusu kikundi cha kigaidi kilichoitwa Namba One. Kikundi hiki kilikuwa na makao yake makuu nje ya Dodoma, katika pori la Namba One, kama unaelekea Iringa. Lilifanya shughuli zake ndani na nje ya Dodoma hadi siku moja mkubwa wake alipokamatwa; na baadaye kupata adhabu ya kifungo cha maisha jela kilichoambatana na kazi ngumu, katika gereza lenye ulinzi mkali la mkoani Shinyanga.
  • 5. Baada ya hapo, viongozi wote wakubwa wa kikundi hicho walikamatwa na kukabidhiwa vifungo kulingana na makosa waliyoyafanya.
  • 6. Nini kilikusukuma kuwa mwandishi wa vitabu? Nilihamasishwa na watu wengi na matukio mengi kuwa mwandishi wa vitabu: Ngugi wa Thiong’o, Ben Mtobwa, Euphrase Kezilahabi, Penina Mlama, Shafi Adam Shafi, sinema za mapigano kama vile The Big Boss ya Bruce Lee na Missing in Action ya Chuck Norris, hadithi kutoka kwa wazee na watu wengine wakubwa, na kadhalika.
  • 7. Hata hivyo, hamasa kubwa zaidi kushinda zote ilitoka kwa Shaaban Robert – mzalendo wa kweli wa Tanzania na kinara wa lugha ya Kiswahili – ambaye vitabu vyake vilinipa nguvu (na tumaini) kuandika riwaya yangu ya kwanza ya Kolonia Santita, ambayo awali iliitwa Salina Cruz.
  • 8. Salina Cruz ni mji wa mwambao wa kusini-magharibi mwa Meksiko, katika jimbo la Oaxaca, kateli ya Kolonia Santita ilipoanzishwa.
  • 9. Nilipomaliza masomo yangu ya sekondari mwaka 1992 nilianza kuandika Kolonia Santita. Kipindi hicho nilikuwa nikisubiri majibu ya mtihani wa taifa wa kidato cha nne. Siku moja (nilipoanza rasmi kuandika, miaka 23 iliyopita) niliijiwa ghafla na ndoto ya mchana nikiwa katika bustani ya nyumbani kwetu Kijitonyama, Dar es Salaam. Vita kubwa ya mawazo iliendelea kichwani mwangu kwa muda mrefu bila kukoma, kuhusiana na dhana fulani ambayo nilikuwa bado sijaielewa sawasawa.
  • 10. Ndoto hiyo ikawa msingi wa taaluma yangu ya uandishi wa vitabu na msingi wa utetezi wangu wa lugha ya Kiswahili. Ikanikumbusha uzuri wa kipaji na uwezo wa talanta nilivyopewa na Mungu na jinsi gani nivitumie, na ikanikumbusha jinsi gani nilivyoweza kuwa na uwezo mkubwa kuburudisha na kuelimisha watu kwa nguvu ya neno.
  • 11. Ujasiri wa kujaribu au jeuri ya kufanya kitu na kujiamini na tumaini, ulinipa msingi wa kufikiri vyema na kuandika kwenye karatasi dhana mbalimbali na mawazo kadha wa kadha kutoka katika dunia niliyoigundua. Nilikuwa na uwezo, nilidhani, wa kuwa mojawapo kati ya watoa burudani bora na waandishi bora wa vitabu Tanzania.
  • 12. Bustanini nilitamani sana kuchapisha kitabu changu nje ya Tanzania na Afrika, mathalani Uingereza au Marekani, ambapo uchapishaji wa vitabu ni wa kimataifa na wa daraja la kwanza. Kichwa changu kilifikiria riwaya ambayo ingesimulia mandhari ya miji zaidi ya minne ulimwenguni kote, ambayo baadaye ingekuwa ya kwanza kwa mauzo hapa Afrika ya Mashariki na Kati.
  • 13. Nilitamani hadithi yangu ichapishwe nje kupata ubora wa kitabu, na ubora wa huduma za uchapishaji wa vitabu.
  • 14. Hadithi ya Kolonia Santita niliiandika kwa miezi mitatu mfululizo hadi nilipokamilisha rasimu ya kwanza kabisa ya muswada wenyewe. (Nilikuwa na umri wa miaka 20 nilipofanya hivyo). Kila nilipodhani muswada umekamilika ili niupeleke kwa wachapishaji, niligundua bado ulihitaji marekebisho.
  • 15. Mwaka 1999 hata hivyo nilidhani umekamilika, na niliupeleka Popular Publications Ltd (PPL) kwa ajili ya mkataba wa uchapishaji wa vitabu. Lakini PPL waliukataa muswada huo. Waliukataa kutokana na ripoti iliyokuwa na mchango mkubwa kwangu ya Hayati Saifu D. Kiango, ambaye kipindi hicho alikuwa mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Tanzania (BAKITA).
  • 16. Kiango alishauri katika ripoti yake masahihisho mengi katika muswada wangu, ambayo yote nilikubaliana nayo, kabla sijaurudisha kwa wachapishaji lakini nikashindwa kufanya hivyo. Nilishindwa kuurudisha kwa wachapishaji.
  • 17. PPL walipoteza baadhi ya sura za muswada wa Kolonia Santita (sura ya 7, 8 na 9) na sikufurahishwa na majibu niliyopewa na Ndg. Mhando (nimesahau majina yake mengine) kwamba yeye/ofisi hawakujua hizo sura zilipokwenda na kwamba yeye/ofisi walipeleka muswada BAKITA ukiwa umekamilika kabisa. Mhando alikuwa mhariri mwandamizi wa PPL.
  • 18. Kwa sababu hiyo niliuondoa muswada wangu PPL na kuweka nadhiri ya kusahihisha kila kosa aliloliona Kiango na kushauri nilisahihishe, na nadhiri ya kuchapisha kitabu hicho mimi mwenyewe nje ya Afrika kama ningepata nafasi.
  • 19. Mnamo mwaka 1992 hadi 1999 nilipata nafasi ya kuandika miswada mingine mitano. Miwili kati ya miswada hiyo ilikuwa imekamilika. Mitatu ilikuwa bado. Mitatu ni ya kipelelezi. Miwili ni ya kimapenzi. Septemba 2004 nilihamia London nchini Uingereza. Huko nilipata nafasi nzuri zaidi ya kufanya utafiti yakinifu, wa miswada yangu yote sita, kwa kiwango nilichokitaka.
  • 20. Katika maisha yangu yote nilitamani sana kuwa mtetezi wa lugha na utamaduni wa Kiswahili. Nadhani tunahitaji wote kuwa watetezi wa lugha hii na lugha zingine za Kiafrika kwani hizi ndiyo utambulisho wa bara letu.
  • 21. Kutokana na hamu hiyo, mwaka 1995 niliweka nadhiri ya kupigania lugha ya Kiswahili maisha yangu yote yaliyobakia. Lakini nilijua hilo lisingewezekana bila kwanza kufanikisha elimu.
  • 22. Mwaka 2010 nilijiunga na chuo cha ubunifu wa kifasihi cha Manchester (The Writers Bureau) nchini Uingereza, kwa lengo la kutimiza ndoto zangu na kupata taaluma ya uandishi wa vitabu. The Writers Bureau walinipa moyo wa kujiamini. Nilikuwa nikiishi shimoni, gizani. Hata hivyo, baada ya kupitia vitabu vichache vya kozi niliona nuru upande wa pili wa tobwe.
  • 23. Nilijua, kutokea kipindi hicho kwamba, endapo ningesoma kwa bidii ningepata uzoefu na utaalamu na mwongozo hasa niliyoutaka. Nilitamani kuwa mwandishi bora wa vitabu na nilitamani kuwaelimisha watu na kuwaburudisha pia. Nilitamani kuwa mojawapo ya waandishi bora wa vitabu na wauzaji bora wa vitabu nchini Tanzania, na nje ya hapo.
  • 24. Ulishindaje? Habari ya Tuzo ya Kiswahili ya Mabati-Cornell ya Fasihi ya Kiafrika niliipata kwa mshangao mkubwa. Kwanza, niliipata kutoka kwa Mkurugenzi wa CDEA (Culture for Development East Africa) Ayeta Anne Wangusa mwezi wa tatu 2015 ofisini kwake Dar es Salaam. Kisha nikaandaa muswada wangu vizuri na kuutuma kupitia tovuti ya tuzo kwa waamuzi wa tuzo, kwa ajili ya mashindano.
  • 25. Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Tuzo ya Kiswahili ya Mabati-Cornell ya Fasihi ya Kiafrika Profesa Abdillatif Abdalla aliponipigia simu kunijulisha kwamba muswada wangu ulishinda nafasi ya pili nilifurahi sana. Nilifurahi sana kiasi kwamba nilijifungia chumbani kwangu hotelini na kucheza muziki kwa masaa matatu mfululizo, na nimekuwa na furaha kuanzia kipindi hicho na kuendelea.
  • 26. Sababu kubwa ya muswada wangu kushinda ni kujitahidi kwa kadiri ya uwezo wangu WOTE. Ni uvumilivu, uchapakazi na nidhamu.
  • 27. Nini ushauri wako kwa waandishi chipukizi? Ushauri wangu pekee ninaoweza kutoa kwa waandishi chipukizi ni elimu! Hutaweza kufikia malengo yako kikamilifu bila msaada wa wataalamu – Hata kama una kipaji au ujuzi kiasi gani.
  • 28. Ukiwa na kipaji nenda shule kurekebisha kipaji chako, ukiwa na ujuzi nenda shule kurekebisha ujuzi wako.